Yeah!
Black market!
Ringle Beatz!
VERS 1
VERS 1
Nakurupuka
kitandani baada ya ndoto za kutisha
Moyo unadunda sana na jasho linanitiririka
Macho nafikicha, taswira, naona kiza
Kwa muda nasizi kimya na dakika zinapita
Zikijirudia ndoto
hatari naona woga Nakosa hoja napotafakari nilichoota Namwamsha wife
aniwekee maji ya kuoga Ananijibu anahisi homa
na mwili mzima umechoka Nampa pole,
Staki kuanzisha zogo wala nini
Maana hata sura inaonesha ana kinyongo na mimi
Ni muda sasa
napokua nae hajiamini
Nacheki saa nagundua nimechelewa kazini
Napiga zangu maji
mwilini And just for the record,
Mimi ndo mtunza funguo za ofisini Nakuta
wafanyakazi na bosi wapo getini Kwa ghadhabu kila mmoja akinitazama
mimi kabla
sijameza mate wala sijabuni sala Naambiwa walikuja wazabuni kwa biashara Na
kwakua nilichelewa kufungua ofisi Mchongo ukafa, nimeingizia kampuni hasara
Baada ya masaa kibao ya kufikiri Ofisi ikaweka kikao kunijadili Waliniona
driver nimeangusha basi Wakafikia mwafaka wakunifukuza kazi Nikatahamaki,
sikujua lakufanya Pale kwenye kamati
hakuna wa kumtazama Nikahisi ni mipango ya
kikuda imefanywa
Sio gari tu, maana hata nyumba nilinyang'anywa
Nikajiuliza
huruma imekwenda wapi? Kila mtu alijua kua nilipenda kazi
Niliheshimu kama
navyoheshimu ndoa ama mzazi Ama muumba,
leo nimepata doa kwenye shati Acha
familia,
vipi deni la ofisi Wamenipa mwezi, nikifeli watanifilisi
Mtoto shule,
pia bunju nina shamba la kukopa
Sijalipa na kijiji nina ndugu wa kutosha Nguvu
zilimalizika,
nikatoka kwa adabu Licha ya ghadhabu kunishika
Nikajipa moyo kua
nna mikono pia na miguu Vyote vyangu
sina sababu ya kushindwa Nilikosa wa
kunishika
wa kumweleza Mshahara ulikua mdogo nilishindwa kuwekeza
Nikapiga moyo
konde mimi mwanaume nita-fight
Nikpanda gari nikampe taarifa wife Nikiwa ndani ya
dimbwi la mawazo Nikitafakari hivi vitimbi na vikwazo Mbele yangu akakatiza
mpita njia Kwakua sikua makini na gari nikamvamiA
Dakika mbili, wananchi
wakalizunguka gari Wakinishutumu sana sababu ya mwendo mkali Nikaitikia wito
nikitegemea thawabu Nikampeleka mgonjwa na akaanza matibabu
Narudi zangu home,
misemo ya kishenzi
nikitema chumbani nasikia mihemo ya mapenzi
Bila hodi,
mlango nikaufungua kwa ghadhabu Nikamkuta
house-boy juu ya kifua cha mke wangu!
Nikabaki kama zuzu
Yule wa kunifariji ndio ameniletea uchungu Nilitaka
nilianzishe
sikua na nguvu Huku nafsi inanishauri kwamba nimwachie Mungu
Swalini kwamba sina moyo mkunjufu? Au kwakua muda sijaenda kuabudu? Au tuseme
mja nina gundu?
Au kwakua nilijenga nyumba na sikuwajulisha ndugu?
Sijaona
faida ya pato langu Wazazi walikufa bila kula jasho langu Mawazo kwenye kichwa
yamezidi Dunia ina watu wengi na sioni \wa kunifariji Naitazama ardhi, naitazama
mbingu Sioni nuru nachoona ni maumivu Maswali mengi, bila majibu Ila Swali
kubwa ni vipi mimi nitaimaliza siku? Jua linazama bado sijiamini Naona
nadondoka ila sioni nikifika chini Saa tano na dakika hamsini Bado dakika kumi
siku iishe na sijui kinafata nini Oh my God


