A.Y tangu alipo kuwa
mototo alijihusisha na maswala ya muziki alipo kuwa shule ya msingi alikuwa
akishiliki katika matamasha mbali mbali ya kutafuta vipaji na pia alitumbuiza
katika halfa mbali mbali. Mnamo mwaka 1996 akiwa high school aliunda kundi la
S.O.G lililo jumuisha wasanii wa tatu
akiwepo yeye mwnyewe katika hilo kundi na wenzake wa wili
Mwaka 2005,AY
alitoa albamu yake ya pili aliyoipa jina ‘Hisia Zangu’, na ‘Yule’, single ya
kwanza kutoka katika albamu hiyo, ilikamata chati mbalimbali za muziki.Katika
albamu hii,AY aliwashirikisha wasanii mbalimbali maarufu katika Afrika
Mashariki ikiwa ni pamoja na Prezzo,Tattuu na Dexu Vultures (wote kutoka Kenya)
na msanii Maurice Kirya kutoka Uganda.Hii ilisaidia sana kumtangaza zaidi AY
nje ya mipaka ya Tanzania.Single yake ya pili, ‘Binadamu’,ilifanya vizuri sana
ukanda mzima wa Afrika Mashariki na hatimaye kuteuliwa kugombea Tuzo za
Kora,jambo lililoandika historia kwani AY ni msanii wa kwanza wa kiume kutoka
Tanzania kuteuliwa kugombea Tuzo hiyo
Umaarufu wa AY ulizidi kuongezeka hasa baada ya kutoa albamu
hiyo ya pili,na sasa alitambulika kama mmoja wa wasanii mahiri wa Afrika
Mashariki.Mwaka 2006 alifanikiwa kupata mkataba wa kutangaza kinywaji (kikali)
cha ‘Konyagi’ ambacho ni maarufu ndani na nje ya Tanzania.Mkataba huo
ulichangia AY kutambulika zaidi kupitia matangazo ya kinyaji hicho,na ulifungua
njia kwa makampuni mengine,kama Coca Cola,Vodacom,Celtel (sasa Tigo) na
Kilimanjaro Lager kuingia mikataba na msanii huyo




No comments:
Post a Comment