UJINGA NENDA Hapa ni
mahali ambapo mtu unajifunza elimu mbali mbali
Na leo nimekuletea umuhimu wa kunywa maji asilimia kubwa ya w Tanzania sio watu wa
kupenda kunywa maji na maji hunjwa pale tu wanapo maliza kula ukitaka kujua
ukweli wa haya maneno
Mtoe rafiki yako katika matembezi mkifika mahali pa kupata
maulaji mulize ni kuagizie maji au soda utasikia jibu atakalo kuambia. Na hapo ndipo huta
amini msemo wangu
Lakini Maji ni muhimu sana kwa afya yako, ukinywa maji kwa siku katika
kiwango kinachotakiwa kiafya utaondokana na matatizo mengi ambayo mengine
ungelazimika kutumia dawa mfano vidonge vya kupunguza maumivu (pain killers) na
matatizo mengine yanayohusiana na uchovu wa mwili.
Kabla sijaorodhesha faida mbalimbali ni vizuri ujue, je kama ukipungukiwa na maji mwilini ni athari au mataizo gani unayopata? Ukipungukiwa na maji mwilini unaweza kujisikia uchovu, kichwa kuuma, ngozi kukakamaa kutokana na kukauka, chakula kutosagwa vizuri ambapo unaweza pata shida kujisaidia haja kubwa nakadhalika.
Vilevile kama ukipungukiwa na maji mwilini utaweza kuwa na hizi dalili.
- Kuhisi kiu au wakati mwingine hata kwikwi.
·
Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya
kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi njaa ni
dalili ya kutakiwa kunywa maji.
·
Je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (ikiwa glasi 1 ina ujazo wa 250ml) sawa na lita 2 kwa siku.
Picha ya glass 6 za maji
Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili
Hizi ni tabia nzuri za kiafya za kuzizingatia.
- Kila uamkapo asubuhi kunywa angalau glasi moja (1) ya maji.
- Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.
Kabla ya kuanza kufanya mazoezi pendelea
kunywa maji kwanza. Kunywa maji glasi 1 au 2 dakika 30 kabla ya kuanza kufanya
mazoezi.
Maji huboresha ngozi.
Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya utendaji kazi mzuri wa kazi zake ikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuonekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha kila siku kuboresha afya ya ngozi yako.

1.
Maji husaidia usagaji wa
chakula.
Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula (digestive system) hutegemea sana maji katika ulainishaji wa chakula na hivyo kuwezesha virutubisho vya chakula kutumika vizuri na mwili, kwakuwa maji hulainisha chakula, pia huepusha kupata choo kigumu (constipation). 2 Maji husaidia kuondosha sumu na taka mwilini.
Licha ya maji kuwa ni sehemu kubwa ya miili yetu pia ni kitu ambacho kinawezesha viungo vingine muhimu kama moyo katika usukumaji damu yenye kiwango kikubwa cha oxygen ambayo inabeba maligafi nyingi na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika ini na kwenye figo ambapo uchujaji wa taka mwilini hufanyika.

3.
Maji husaidia kupunguza
maumivu mbalimbali kama ya kichwa pamoja na mgongo.
Licha ya kuwa na sababu nyingi za mtu kupata maumivu ya kichwa lakini pia ukosefu wa maji mwilini ni sababu moja wapo ya kichwa kugonga kwasababu ya kupungukiwa na mahitaji muhimu kama oxygen ambayo husafirishwa na damu ambapo maji husaidia kurahisisha shughuli hizo.
4Maji huusaidia mwili kupigana na magonjwa mengi kama ya mafua, tumbo, saratani za aina mbalimbali na matatizo mengine ya figo.
Maji pamoja na juisi ya malimao husaidia sana kupooza magonjwa kama ya kikohozi, mafua, kuchafuka kwa tumbo, satani ya tumbo na kibofu cha mkojo nakadhalika. Maji yanaweza kukuepusha au kupunguza makali ya magonjwa hayo kwa kusaidia mwili wako kuongeza kinga ya mwili.
5. Maji husaidia kupunguza uzito.
Kama nilivyosema hapo awali wakati mwingine unaweza hisi kuwa unahitaji kula kumbe unahitaji kunywa maji kwakuwa umepungukiwa na maji mwilini. Ni mara ngapi umekuwa ukitamani kula chakula kwa pupa lakini baada ya kunywa maji ukajikuta unakula kidogo kuliko ulivyotegemea hapo awali.
Uzito wa mwili hutegemea sana ulaji wa chakula pasipo kufanya mazoezi, maji pia husaidia kuondoa taka za vyakula vya mafuta (fats by-products) na kukuwezesha uwe mwenye afya bora.

6. Maji husaidia kuboresha misuli na kulainisha jointi za viungo vya mwili.
Maji ni chanzo cha nguvu mwilini, misuli huifadhi nguvu ya ziada itakayotumika iwapo nguvu ya mwili itapungua. Kunywa maji kulingana na mahitaji ya mwili wako ili kuwezesha utumikaji mzuri wa chakula na uhifadhi wa uhakika wa nguvu mwilini. Maji pia yatakusaidia kulainisha viungo vyako vya mwili kama jointi za kwenye magoti, vidole vya mikono na miguu
Imendikwa na kuandaliwa na keytus define

No comments:
Post a Comment