Pages - Menu

follow

21/09/2015

PIGO KAMPUNI YA APPLE YAVAMIWA KIMTANDAO


Kampuni ya Apple ya Marekani imesema kuwa ipo katika hatua za kukabiliana na shambulio la kimitandao,ambapo wamebaini kuwa program hatari ya kimitandao iliyopo kwa watumiaji wa simu za IPhone na iPad nchini China.
Watalaam wa ndani ya kampuni hiyo wamesema kuwa inaelezwa kuwa hili ni moja la shambulio kubwa la kimitandao kuwahi kuikumba kampuni hiyo.
Apple wanasema kwua wavamizi hao wa kimitandao wanasema wamebuni namba za siri ambazo huwawezesha watumiaji wa vifaa hivyo vya Apple kuingiziwa programu zinazoathiri mawasiliano yao.
Msemaji wa Apple anasema kuwa kampuni yao imeondoa kwenye mzunguko wa soko vifaa vyote vinavyotiliwa shaka kuingiliwa na wavamizi hao wa kimitandao nchini China.

05/09/2015

maneno ya kejeri


FAIDA YA MAJI

UJINGA NENDA  Hapa ni mahali ambapo mtu unajifunza elimu mbali mbali
Na leo nimekuletea umuhimu wa kunywa maji  asilimia kubwa ya w Tanzania sio watu wa kupenda kunywa maji na maji hunjwa pale tu wanapo maliza kula ukitaka kujua ukweli  wa haya maneno
Mtoe rafiki yako katika matembezi mkifika mahali pa kupata maulaji mulize ni kuagizie maji au soda utasikia  jibu atakalo kuambia. Na hapo ndipo huta amini msemo wangu
Lakini  Maji ni muhimu sana kwa afya yako, ukinywa maji kwa siku katika kiwango kinachotakiwa kiafya utaondokana na matatizo mengi ambayo mengine ungelazimika kutumia dawa mfano vidonge vya kupunguza maumivu (pain killers) na matatizo mengine yanayohusiana na uchovu wa mwili.

Kabla sijaorodhesha faida mbalimbali ni vizuri ujue, je kama ukipungukiwa na maji mwilini ni athari au mataizo gani unayopata? Ukipungukiwa na maji mwilini unaweza kujisikia uchovu, kichwa kuuma, ngozi kukakamaa kutokana na kukauka, chakula kutosagwa vizuri ambapo unaweza pata shida kujisaidia haja kubwa nakadhalika.

Vilevile kama ukipungukiwa na maji mwilini utaweza kuwa na hizi dalili.
  • Kuhisi kiu au wakati mwingine hata kwikwi.
·         Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kunywa maji.
·          

Je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (ikiwa glasi 1 ina ujazo wa 250ml) sawa na lita 2 kwa siku.
Picha ya glass 6 za maji



Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili
Hizi ni tabia nzuri za kiafya za kuzizingatia.
  • Kila uamkapo asubuhi kunywa angalau glasi moja (1) ya maji.
  • Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.
Kabla ya kuanza kufanya mazoezi pendelea kunywa maji kwanza. Kunywa maji glasi 1 au 2 dakika 30 kabla ya kuanza kufanya mazoezi.

Maji huboresha ngozi.

Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya utendaji kazi mzuri wa kazi zake ikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuonekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha kila siku kuboresha afya ya ngozi yako.



1.    Maji husaidia usagaji wa chakula.

Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula (digestive system) hutegemea sana maji katika ulainishaji wa chakula na hivyo kuwezesha virutubisho vya chakula kutumika vizuri na mwili, kwakuwa maji hulainisha chakula, pia huepusha kupata choo kigumu (constipation).
 2 Maji husaidia kuondosha sumu na taka mwilini.

Licha ya maji kuwa ni sehemu kubwa ya miili yetu pia ni kitu ambacho kinawezesha viungo vingine muhimu kama moyo katika usukumaji damu yenye kiwango kikubwa cha oxygen ambayo inabeba maligafi nyingi na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika ini na kwenye figo ambapo uchujaji wa taka mwilini hufanyika.
3.    Maji husaidia kupunguza maumivu mbalimbali kama ya kichwa pamoja na mgongo.

Licha ya kuwa na sababu nyingi za mtu kupata maumivu ya kichwa lakini pia ukosefu wa maji mwilini ni sababu moja wapo ya kichwa kugonga kwasababu ya kupungukiwa na mahitaji muhimu kama oxygen ambayo husafirishwa na damu ambapo maji husaidia kurahisisha shughuli hizo.
4Maji huusaidia mwili kupigana na magonjwa mengi kama ya mafua, tumbo, saratani za aina mbalimbali na matatizo mengine ya figo.

Maji pamoja na juisi ya malimao husaidia sana kupooza magonjwa kama ya kikohozi, mafua, kuchafuka kwa tumbo, satani ya tumbo na kibofu cha mkojo nakadhalika. Maji yanaweza kukuepusha au kupunguza makali ya magonjwa hayo kwa kusaidia mwili wako kuongeza kinga ya mwili.

5. Maji husaidia kupunguza uzito.

Kama nilivyosema hapo awali wakati mwingine unaweza hisi kuwa unahitaji kula kumbe unahitaji kunywa maji kwakuwa umepungukiwa na maji mwilini. Ni mara ngapi umekuwa ukitamani kula chakula kwa pupa lakini baada ya kunywa maji ukajikuta unakula kidogo kuliko ulivyotegemea hapo awali. 


Uzito wa mwili hutegemea sana ulaji wa chakula pasipo kufanya mazoezi, maji pia husaidia kuondoa taka za vyakula vya mafuta (fats by-products) na kukuwezesha uwe mwenye afya bora.

6. Maji husaidia kuboresha misuli na kulainisha jointi za viungo vya mwili.

Maji ni chanzo cha nguvu mwilini, misuli huifadhi nguvu ya ziada itakayotumika iwapo nguvu ya mwili itapungua. Kunywa maji kulingana na mahitaji ya mwili wako ili kuwezesha utumikaji mzuri wa chakula na uhifadhi wa uhakika wa nguvu mwilini. Maji pia yatakusaidia kulainisha viungo vyako vya mwili kama jointi za kwenye magoti, vidole vya mikono na miguu

                                                                                 
                                                             Imendikwa na kuandaliwa na keytus define

POMBE ZINAZIDI KUMPONZA ARTURO VIDAL


Nidhamu ni kitu cha msingi sana kwenye kazi yoyote zaidi ya uwezo wako ulionao kwenye kufanya hiyo kazi. Vidal hivi sasa kafukuzwa na kocha wake Jorge Sampaoli arudi kupumzika hadi atakapo kuwa fit.
Chile ipo kwenye mazoezi ikitegemea kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Paraguay. Wachezaji wapo pamoja kwa ajili ya mazoezi lakini Vidal aliripoti kwenye kambi ya timu ya taifa Jumanne mchana akiwa bado ana pombe kichwani mwake. Kocha Sampaoli alimrudisha na kumwambia arudi Ujerumani hadi pale atakapo kuwa tayari. Kocha huyo pia alimpa onyo kali mchezaji huyo kwamba anampa nafasi ya mwisho.
Vidal aliwai kuhatarisha maisha yake na ya mpenzi wake baada ya kupata ajali ya Ferrari baada ya kunywa pombe usiku mkali huko Santiago. Baada ya kuomba msamaha kwa machozi akaruhusiwa kujiunga tena na Chile na kushinda Copa America.
Chama cha soka cha Chile kimetoa statement kwamba Vidal karudishwa ujerumani kwasababu ya matatizo yake binafsi.

JINSI YA KUTUMIA COMPUTER KUENDESHA SIMU YAKO YA ANDROID

Android inazidi kuwafurahisha watumiaji wa simu za android kila kukicha kwa kuifanya android izidi kuwa mbele daima. Sasa android imekuja na kitu kipya ambacho inakuwezesha kuiendesha simu yako kwa kutumia computer. Hii ni kweli na sio utani kwamba utaweza kuiamisha simu yako ya android na kuonekana kwenye computer na utaweza kutuma email, kucheza game, kutuma message na mambo mengine mengi kwa kutumia computer




JINSI YA KUTUMIA COMPUTER KUENDESHA SIMU YAKO YA ANDROID

STEP 0

Download android Usb drivers kwa kupitia link chini kisha install kwenye computer yako.
http://download.clockworkmod.com/test/UniversalAdbDriverSetup.msi

STEP 1

Nenda kwenye settings ya simu yako tazama kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyoonekana chini Note
Endapo Developer Options itakuwa haipo kwenye settings, nenda kwenye about phone kisha nenda kwenye kipengele kinachosema build number kisha ki bonyeze kama mara sita au saba kisha rudi tena kwenye settings halafu angalia kama developer options imetokea.





STEP 2

Ndani ya developer options hakiki ipo on na weka tick kwenye kipengele kinachosema Enable USB DEBUGGING kama picha inavyoonekana chini


STEP 3

Kwnye computer fungua browser ya chrome. Tembelea link chini kisha bonyeza kipengele kilichoandikwa ADD TO CHROME
https://chrome.google.com/webstore/detail/vysor-beta/gidgenkbbabolejbgbpnhbimgjbffefm?authuser=1


Endapo utafanikiwa utapata message kama yenye ujumbe kama picha chini


STEP 4

Baada ya hapo  nenda kwenye computer tafuta program inayoitwa chrome app launcher ambayo inakuwaga kwenye taskbar. Fngua chrome app launcher kisha click program inayoitwa vysor.

STEP 5

Chomeka usb cable kwenye simu yako na kwenye computer. Endapo utapata ujumbe kama picha chini kwenye simu yako, hakikisha unasema ok

Hapo hapo utaona kwenye computer yako simu yako imeunganishwa na utapata ujumbe kama picha inavyoonekana chini kwenye simu yako

25/08/2015

DIZASTA VINA-SIKU MBAYA

Yeah!
 Black market!
 Ringle Beatz!
VERS 1
Nakurupuka kitandani baada ya ndoto za kutisha
 Moyo unadunda sana na jasho linanitiririka
 Macho nafikicha, taswira, naona kiza
 Kwa muda nasizi kimya na dakika zinapita
Zikijirudia ndoto hatari naona woga Nakosa hoja napotafakari nilichoota Namwamsha wife
 aniwekee maji ya kuoga Ananijibu anahisi homa
 na mwili mzima umechoka Nampa pole,
 Staki kuanzisha zogo wala nini
 Maana hata sura inaonesha ana kinyongo na mimi
Ni muda sasa napokua nae hajiamini
 Nacheki saa nagundua nimechelewa kazini
Napiga zangu maji mwilini And just for the record,
 Mimi ndo mtunza funguo za ofisini Nakuta wafanyakazi na bosi wapo getini Kwa ghadhabu kila mmoja akinitazama
mimi kabla sijameza mate wala sijabuni sala Naambiwa walikuja wazabuni kwa biashara Na kwakua nilichelewa kufungua ofisi Mchongo ukafa, nimeingizia kampuni hasara Baada ya masaa kibao ya kufikiri Ofisi ikaweka kikao kunijadili Waliniona driver nimeangusha basi Wakafikia mwafaka wakunifukuza kazi Nikatahamaki,

 sikujua lakufanya Pale kwenye kamati
 hakuna wa kumtazama Nikahisi ni mipango ya kikuda imefanywa 
Sio gari tu, maana hata nyumba nilinyang'anywa
 Nikajiuliza huruma imekwenda wapi? Kila mtu alijua kua nilipenda kazi
 Niliheshimu kama navyoheshimu ndoa ama mzazi Ama muumba,
 leo nimepata doa kwenye shati Acha familia, 
vipi deni la ofisi Wamenipa mwezi, nikifeli watanifilisi 
Mtoto shule, pia bunju nina shamba la kukopa
 Sijalipa na kijiji nina ndugu wa kutosha Nguvu zilimalizika,
 nikatoka kwa adabu Licha ya ghadhabu kunishika
 Nikajipa moyo kua nna mikono pia na miguu Vyote vyangu
 sina sababu ya kushindwa Nilikosa wa kunishika 
wa kumweleza Mshahara ulikua mdogo nilishindwa kuwekeza 
Nikapiga moyo konde mimi mwanaume nita-fight 
Nikpanda gari nikampe taarifa wife Nikiwa ndani ya
dimbwi la mawazo Nikitafakari hivi vitimbi na vikwazo Mbele yangu akakatiza mpita njia Kwakua sikua makini na gari nikamvamiA
 Dakika mbili, wananchi wakalizunguka gari Wakinishutumu sana sababu ya mwendo mkali Nikaitikia wito nikitegemea thawabu Nikampeleka mgonjwa na akaanza matibabu 
Narudi zangu home, misemo ya kishenzi 
nikitema chumbani nasikia mihemo ya mapenzi
 Bila hodi, mlango nikaufungua kwa ghadhabu Nikamkuta 
house-boy juu ya kifua cha mke wangu! Nikabaki kama zuzu 
Yule wa kunifariji ndio ameniletea uchungu Nilitaka nilianzishe 
sikua na nguvu Huku nafsi inanishauri kwamba nimwachie Mungu Swalini kwamba sina moyo mkunjufu? Au kwakua muda sijaenda kuabudu? Au tuseme mja nina gundu?
 Au kwakua nilijenga nyumba na sikuwajulisha ndugu?
 Sijaona faida ya pato langu Wazazi walikufa bila kula jasho langu Mawazo kwenye kichwa yamezidi Dunia ina watu wengi na sioni \wa kunifariji Naitazama ardhi, naitazama mbingu Sioni nuru nachoona ni maumivu Maswali mengi, bila majibu Ila Swali kubwa ni vipi mimi nitaimaliza siku? Jua linazama bado sijiamini Naona nadondoka ila sioni nikifika chini Saa tano na dakika hamsini Bado dakika kumi siku iishe na sijui kinafata nini Oh my God


17/08/2015

2 CHAIN ATOA MIXTAPE TRAPAVEL TRE

2chain ameachia mix tape yenye nyimbo 16 katika mixtap hii amewataja kuwepo na wasanii wakubwa kama wizkhalifa, the dream,kevin gates na wengineo kwa upande wa productio 2chain amfanya na ma producer wenye majina makubwa katika game kama FKi, Mike Dean, Honorable C-Note, Zaytoven, Nard & B, TM-88, and Murda Beatz na wengineo

unaweza ukaisikiliza na kuidownload bule na hii ndo list ya nyimbo zilizo kuwepo kwenye hii mixtape
Tracklist
01. DJ Bigga Rankin Intro
02. Neighborhood (Prod. By B Wheezy iBeatz Mike Dean X)
03. A Milli Billi Trilli Feat. Wiz Khalifa (Prod. By FKi Murda Beatz)
04. Everything I Know (Prod. By Nard B)
05. Watch Out (Prod. By FKi)
06. BFF (Prod. By Zaytoven)
07. I Feel Like Feat. Kevin Gates (Prod. By Hitmakah Arch tha Boss)
08. GOAT Feat. The Dream (Prod. By Bwheezy Mike Dean)
09. Halo Letter From My Unborn Son Feat. Heaven Harmony (Prod. By Street Symphony 808xElite)
10. Big Meech Era (Prod. By TM88)
11. Starter Kit Feat. Young Dolph (Prod. By Zaytoven)
12. If I Didn t Rap (Prod. By Fresh Jones)
13. El Chapo Jr (Prod. By Two7teen)
14. Lapdance In The Trap House (Prod. By Honorable C Note)
15. Each Erry One Of Em Feat. Cap 1 Skooly (Prod. By Honorable C Note)
16. Blue Dolphin Feat. Betty Idol (Prod. By Nard B)

16/08/2015

LIKE FATHER LIKE SON REMIX


AMBWENE ALLEN YESSAYA (A.Y)

Abwne allen yessaya alizaliwa julai 5 1981jina la stage anajulikana kama A.Y ni mwanamuziki anaye fanya mzik wa komesho,rap na hip hop PIA ni muigizaji na mwanamitindo  kutokea nchi ya Tanzania

A.Y  tangu alipo kuwa mototo alijihusisha na maswala ya muziki alipo kuwa shule ya msingi alikuwa akishiliki katika matamasha mbali mbali ya kutafuta vipaji na pia alitumbuiza katika halfa mbali mbali. Mnamo mwaka 1996 akiwa high school aliunda kundi la S.O.G  lililo jumuisha wasanii wa tatu akiwepo yeye mwnyewe katika hilo kundi na wenzake wa wili

Mwaka 2005,AY alitoa albamu yake ya pili aliyoipa jina ‘Hisia Zangu’, na ‘Yule’, single ya kwanza kutoka katika albamu hiyo, ilikamata chati mbalimbali za muziki.Katika albamu hii,AY aliwashirikisha wasanii mbalimbali maarufu katika Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Prezzo,Tattuu na Dexu Vultures (wote kutoka Kenya) na msanii Maurice Kirya kutoka Uganda.Hii ilisaidia sana kumtangaza zaidi AY nje ya mipaka ya Tanzania.Single yake ya pili, ‘Binadamu’,ilifanya vizuri sana ukanda mzima wa Afrika Mashariki na hatimaye kuteuliwa kugombea Tuzo za Kora,jambo lililoandika historia kwani AY ni msanii wa kwanza wa kiume kutoka Tanzania kuteuliwa kugombea Tuzo hiyo
 Umaarufu wa AY ulizidi kuongezeka hasa baada ya kutoa albamu hiyo ya pili,na sasa alitambulika kama mmoja wa wasanii mahiri wa Afrika Mashariki.Mwaka 2006 alifanikiwa kupata mkataba wa kutangaza kinywaji (kikali) cha ‘Konyagi’ ambacho ni maarufu ndani na nje ya Tanzania.Mkataba huo ulichangia AY kutambulika zaidi kupitia matangazo ya kinyaji hicho,na ulifungua njia kwa makampuni mengine,kama Coca Cola,Vodacom,Celtel (sasa Tigo) na Kilimanjaro Lager kuingia mikataba na msanii huyo

15/08/2015

S JIZZO ACHIA NGOMA NYINGINE MPYA

S jizzo aja na ngoma nyinge baada ya kuachia nyimbo ya pesa shilingi sasa haja na hii ya YAKO WAPI alioifanya kwa BOMA RECORD


S JIZZO-PESA SHILINGI

                   Msanii chipukiz anaye kuja vizur kunako game ya bongo fleva  S JIZZO FT BELLECA 

08/08/2015

MJUE MIRADI AYO HAPA

MIRADI AYO
Ni mtangazji wa tv  na redio station  pia ana run website yake mwenyewe inayo julikana kwa “miradi ayo”
Amekuwa ni mtangazaji mwenye ushawaishi mkubwa kwa vijana na kuwa mfano wa kuiigwa

Miradi ayo amezaliwa na kusoma elimu yake mkoani Arusha kabla ya kujiunga na chuo cha utangazaji EAST AFRICA TRANING INSTITUTE
Ila kwa upande wa darasani miradi ana kili hakuwa mzuri kiasi cha kufikia hatua ya kuamini pengine ye maisha yake hayako upande wa elimu
CHANGAMOTO
Akizungumza na blog hii miradi anasema “kipindi ambacho kilikuwa kigumu ni pale baba yangu alipopata ajari ya gar ambalo alikuwa akilitegemea kuingizia kipato uchumi ukayumba sana pale nyumbani ” 

MTU MABAYE ATAMSAHAU
Mtangazaji huyo mwenye sauti ya kipekee akiwa hewani anasema  mtu ambaye hatokuja kumsahau katika maisha yake ni mjomba wake gablier robart ambaye alikuwa ametokea malekani na kufikia pale home na kuongea na mama wa miradi ayo kuhusu kitu anacho kipenda miradi. nayeye  akachukua jukumu la kumsomesha katika chuo cha utangazaji cha east Africa institute

MAFANIKIO
Miradi ameshinda tuzo za watu mala mbili 2015 katika kipengela cha
Blog/website inayopendwa  na watu miradi ayo.com imeshinda
2014 ameshinda mtangazaji wa redio anayependwa na watu
Ana miliki tv ya online AYO TV ambayo imekuwa gumzo sana
Pia ana mpango wa kufungua radio station yake mwenyewe amesha nunua vifaa bado mambo  madogo  ambayo anayaweka sawa amehaidi kama atakamilisha atatutalifu

UJUMBE KUTOKA KWA MIRADI AYO
Ili ufanikiwe unahitaji kuwa mvumilivu na mchapakazi pamoja na heshima kwa rika zote


We ni wathamani endelea kuwa pamoja na mimi ili kuendelea kupata habari zinapotufika pia usisahau. ku subscribe chanel yangu ya youtube.pamoja na  facebook na  twitter
“Wewe ni wa thamani kwangu”

06/08/2015

Wasanii wamuaga Dr. Jakaya Kikwete na kumkaribisha Dr. John Pombe Magufuli Mlimani City




Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dr. Jakaya Kikwete, Kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh.



Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto, Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli na Mwigizaji Jacob Steven JB wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Mwanamuziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz akiwasili na Meneja wake wa shughuli za kimataifa Bw.Salam.

Davis Mosha (kulia) akiwa pamoja na Mboni Masimba wa The Mboni Show wakiperuzi kwenye simu.




Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Radio.


 
We ni wathamani endelea kuwa pamoja na mimi ili kuendelea kupata habari zinapotufika pia usisahau. ku subscribe chanel yangu ya youtube.pamoja na  facebook na  twitter
“Wewe ni wa thamani kwangu"
 
 



New video

simu tv

simu tv

MPIGIE KURA WAKAZI

MPIGIE KURA WAKAZI