Pages - Menu

follow

11/06/2015

DIZASTA VINA

jina halisi ni edger vicent, jina la kwenye stage anajulikana kama dizasta vina mnyakyusa kutoka mbeya.ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yake na ni mwanaume pekee akiwa na dada zake wawili
 ELIMU alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya kimanga,wilaya ya ilala jijini dar es salaam kabla ya kuendelea na masomo ya sekondari katika shule binafsi ya WHITE LAKE SECONDARY SCHOOL iliyopo eneo la changanyikeni jijini dar es salaam kisha kumaliza masomo ya sekondari katika shule ya SOUTHERN HIGHLAND SECONDARY SCHOOL iliyopo soweto jijini mbeya.aliendelea na masomo ya elimu ya juu katika shule ya KIGOMA BOYS HIGH SCHOOL kabla ya kumalizia katika shule ya MBEYA HIGH SCHOOL na kisha kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika taasisi ya usimamizi wa fedha IFM mwaka 2013.


MUZIKI alipenda mziki tangu akiwa mtoto,anasema "familia yetu inapenda mziki sana,mama na dada zangu wote waliimba kwaya katika vipindi tofauti,na wengine bado wanaimba mapka sasa".alikuwa anakariri nyimbo za wasanii mbalimbali wakubwa hapa Tanzania kama professor jay,afande sele,juma nature na solo thang na hata watu walikuwa wakimpa pesa ili awaimbie baadhi ya nyimbo zilizotamba wakati huo.anasema "nilipata inspiration kubwa kutoka katika album ya MACHOZI JASHO NA DAMU ya   professor jay"
HARAKATI ZA KUTOKA KIMZIKI alijiingiza rasmi katika muziki mwaka 2007 kwa kushiriki katika matamasha na mashindano mbalimbali ikiwemo SM STRAIGHT MUZIK FREESTYLE BATTLE mwaka 2010 mkoani iringa.mwaka 2011 alikutana na producer aliyemwinua duke touchez."duke alinipa mwongozo wa jinsi ya kijiunga na tamadunimuzik ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa inatafuta vipaji vipya kwa ajili ya foundation" dizasta alishiriki mashindano ya kurap katika tamasha la kuachia santuri 5 kwa mpigo (african son ya stereo,sauti ya jogoo ya nikki mbishi,mzimu wa shabaan robert ya nash mc,underground legendary ya duke touchez na mathematrix ya songa na ghetto ambassador) na kufanikiwa kujiunga rasmi na tamadunimuzik.
Nyimbo alizo fanikiwa ku record- mwaka 2012 alifanikiwa kuachia wimbo wake rasmi HARDER  www.mdundo.com/song/12799  na kushiriki katika nyimbo kadhaa za kushirikiana the ultimate     ,sautiyamtaa (http://www.reverbnation.com/dizasta4/song/18691461-mkemia-dizasta-dubo-n-phil-techniques) kwa kipindi cha kati ya mwaka 2012 na 2013.mwaka 2013   aliachia track nyingine iliyokwenda kwa jina la tega sikio www.mdundo.com/song/12837 ,goli la ushindi www.mdundo.com/song/12836  .kisa cha nyumba ndogo www.mdundo.com/song/15974 na sister www.mdundo.com/song/20014 alishiriki kwenye underground project ya producer AK 47 iliyokwenda kwa jina la heavyweight akishirikiana na msanii tifa flows www.mdundo.com/song/12838 pia katika project ya uwezo ya producer ngwesa katik track ya miss tamaduni akishirikiana na jeff duma www.mdundo.com/song/15525 .mwaka huo huo alishiriki katika album ya upande wa pili wa sarafu ya producer abby mp,project ya kilinge ya duke touchez,album ya kiutu uzima ya msanii kadgo,mixtape ya slow jams ya producer innocent mujwahuki,tamaduni foundation ya ngwesa na representing africa popote ya one the incredible


   tayari ameshaachia track mwaka 2015 inayokwnda kwa jina la kijogoo
www.mdundo.com/song/25504 ,ameshirikikatika project ya siku nikifa ya kipepe www.mdunndo.com/song/24731  

     IMANI  dizasta vina  ni muumini wa dini ya kikristu na anaabudu katika dhehebu la kikatoriki,anashiriki katika sala na misa kila  anapopata wakati.anasema "kuna muda utafika muziki hautakuwa mwokozi wako,lazima na tutambue kuwa kuna maisha baada ya kifo hivyo tujiandae"

         NJE YA MUZIKI dizasta VINA  ni mwanafunzi wa mwaka wa pili akichukua stashahada ya kwanza udhamiri katika uhasibu (bachelor degree in accountancy) 2015.ni mpenzi wa mpira wa miguu na ni mshabiki wa kutupwa wa timu ya yanga na arsenal.dizasta ni mpenzi wa mchezo wa kuogelea pia ni muogeleaji mzuri.




PAKUA NYIMBO NYINGINE ZA DIZASTA VINA HAPA

foundation  
www.mdundo.com/song/12840

word play feat shaolin  
www.mdundo.com/song/24733

bado nzito feat one n
dubowww.mdundo.com/song/12839

siku nikifa 
www.mdundo.com/song/24731

kijogoo 
www.mdundo.com/song/25504

goli la ushindi 
www.mdundo.com/song/12836
HANA PATIKANA KATIKA MITANDAO  HII YA KIJAMII
Facebook- dizasta vina
Tweeter-@dizastavina
Instagram-@dizastavina

No comments:

Post a Comment

New video

simu tv

simu tv

MPIGIE KURA WAKAZI

MPIGIE KURA WAKAZI